Alhamisi , 15th Jul , 2021

'Sporst Countdown' ya EastAfrica redio ni kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 1:15 asubuhi katika kuhesabu stori kali 6 zita za kimichezo kuanzia usiku wa kumakia leo, zile zitakazo jiri hapo baada na kesho kupitia kipindi cha 'Super Breakfast'

Haruna Niyonzima wa Yanga akiongea mbele ya wanahabari kuelekea kwenye mchezo wa Yanga dhidi ya KMC mwaka huu.

6 - Ni idadi ya miaka ambayo kiungo fundi raia wa Rwanda, Haruna Niyonzima aliitumikia klabu ya Yanga kwenye ungwe ya kwanza tokea atue klabuni hapo mwaka 2011 kabla ya kuhamia klabu ya Simba mwaka 2017 na kirejea tena Yanga januari mwaka 2020.

Mkali huyo wa machwejo anataraji kuangwa kwa heshima na Uongozi pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wakati Yanga itakaposhuka dimbani saa 10:00 jioni kukipiga na Ihefu ya jijini mbeya kwenye dimba la mkapa Jijini Dsm.

Niyonzima anaondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kandarasi yake kumalizika na mabingwa hao wakihistoria nchini.

5 - Ni miaka ambayo inaelezwa Nyota wa FC Barcelona, Lionel Messi mwenye umri wa miaka 34 amekubali kusaini kuendelea kubakia klabuni hapo Hadi mwaka 2026 kwa kulipwa nusu ya mshahara aliokuwa anapokea wa paundi milioni 123 (zaidi ya bilioni 369 za Kitanzania) kwa mwaka ambapo kwa kuanzia msimu ujao atapokea paundi milioni 61.5 sawa na zaidi ya bilioni 180 za Kitanzania.

Makubaliano hayo ambayo bado hayajawekwa kwenye saini, yamekuja zikiwa zimepita wiki mbili Messi kuwa mchezaji huru kufuatia mkataba wake na miamba hiyo ya soka nchini Hispania kumalizika Juni 30.

Kandarasi hiyo pia inaakisi azma ya nyota huyo kutaka kumalizia soka lake Barcelona na kuendelea kuzidi kuweka rekodi za kibabe tokea aanze kuchezea timu ya wakubwa 2005 na kuwa mchezaji pekee Duniani aliyefunga mabao mengi akiwa na klabu moja pamoja na kushinda tuzo 6 za mchezaji bora wa Dunia.

4 - Ni idadi ya wacheza tennis bora duniani kwa upande wa wanaume watakaokosekana kwenye mashindano ya Tokyo Olympic Julai 24 mwaka huu nchini Japan kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha, na hii ni mara baada ya Mwingereza, Den Evans anayeshikilia nafasi ya 1 nchini humo na ya 28 kwenye viwango vya ubora vya tennis Duniani kuthibitika kuwa atakosekana kwenye mashindano hayo makubwa Duniani kufuatia kupata maambuzi ya Covid-19 usiku wa kuamkia leo.

Den Evans ambaye alishindwa kutinga kuvuka hatua ya 16 bora ya michuano ya Tennis ya Wimbledon iliyomalizika juma lililopita nchini England baada ya kutolewa na Sebastian Korda amesema amesikitishwa na kuumizwa sana na maladhi hayo yanayomnyima kushiriki micha tennis wengine watatu watakaokosekana kwa upande wa wanaume ni, Mhispania, Rafael Nadal anayeshikilia nafasi ya 4, Muastralia, Dominic Thiem aliyepo nafasi ya 6 na Mswiz, Rodger Federer anayeshika nafasi ya 9 kwenye viwango vya ubora vya tennis Ulimwenguni.

3 - Ni idadi ya wachezaji wa kikosi cha Azam watakaokosekana kwenye mchezo wake dhidi ya mabingwa wa ligi kuu klabu ya Simba utakaochezwa saa 1:00 Usiku wa leo kwenye dimba la Chamazi, Jijini Dsm.

Kocha msaidizi wa Azam, Bahati Vivier amethibitisha wachezaji watakaokosekana ni mlinzi na nahodha wa kikosi hicho, Aggrey Moris, kiungo mshambuliaji, Salum Aboubakari 'Sure boy' na mshambuliaji wao tegemezi, Mzimbabwe, Prince Dube ambao wanakosekana kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Nae kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola ameweka wazi kuwa licha ya maandalizi ya mchezo huo kukamilika na kwenda vizuri lakini watawakosa wachezaji wake wanne kutokana na sababu mbalimbali.

Kiungo Jonas Mkude anaendelea kukosekana kutokana na sakata lake la utovu wa nidhamu lililopelekea kusimamishwa klabu hapo tokea mwezi uliopita, winga Bernard Morrison yupo nchini kwao Ghana kutokana na sababu za kifamilia na kutaraji kurejea leo, kiungo Ibrahim Ajib anasumbuliwa na Malaria ilhali Miraji Athumani ana majeraha.

Mbali na mchezo huo, VPL itaendelea leo kwa michezo 8, ukiwemo ule wa Yanga dhidi ya Ihefu utakaochezwa saa 10:00 jioni kwenye dimba la BW Mkapa jijini Dsm.

2 - Ni idadi ya penalti ambazo mlinda mlango Gianluigi Donnarumma alizipangua dhidi ya England na kuipa ushindi wa penalti 3-2 na kuisaidia timu yake ya Italy kuwa mabingwa wa UEFA EUROS 2020.

Shujaa huyo wa Italia amekamilisha usajili wake wa kutoka klabu ya AC Milan na kutua PSG usiku wa kuamkia leo huku akisaini kandarasi ya miaka 5 akiwa mchezaji huru.

Shujaa huyo wa Italia amekamilisha usajili wake wa kutoka klabu ya AC Milan na kutua PSG usiku wa kuamkia leo huku akisaini kandarasi ya miaka 5 akiwa mchezaji huru.

Licha ya Ujio wa kipa huyo anayekuja kwa kasi kwa sasa, timu ya PSG imethibitisha haitomuachia kipa wake chaguo la kwanza wa msimu uliopita Keylor Navas.

1 - Ni idadi ya rebound ambayo nyota wa Phoenix Suns, Devin Booker aliiambulia wakati timu yake ikifungwa kwa alama 109-103 dhidi ya Milwaukee Bucks kwenye mchezo wa nne wa fainali ya NBA nchini Marekani alfajiri ya leo na kufanya wawili hao kutoshana nguvu kwa series 2-2.

Booker alikusanya alama 42 na assist 2 ambazo zimemfanya aibuke kuwa nyota wa mchezo huo na kuwapiku Giannis Antetokounmpo mwenye alama 26, rebound 14 na assist 4 ilhali Khris Middleton alipata alama 40, rebound 6 na assist 4 wa Bucks.

Wawili hao watashuka tena dimbani julai 18 na 21 mwaka huu ili kumsaka mshindi atakayeongoza series 4 na kuwa bingwa wa NBA.