Jumanne , 13th Jul , 2021

Stori sita (6) za michezo (Sports Countdown) leo asubuhi kwenye Supa Breakfast ya East Africa Radio kuanzia Saa 1:15 Asubuhi, ambapo kila stori inatokana na namba 1 mpaka 6. Na moja ya stori ni klabu ya Simba Queens itakabidhiwa ubingwa wa Ligi leo, na Yanga itamuaga Niyonzima Julai 15.

Wachezaji wa Simba Queens watakabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi ya wanawake leo

6. Ni tuzo za mchezaj bora wa Dunia alizoshinda Lionel Messi ambapo kwa sasa inajadiliwa kama mchezaji huyo anastahili kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya saba mwaka huu. Messi anatazamiwa kuwa mstali wa mbele kwenye kinyanganyiro cha kuwania tuzo hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Copa America na timu ya taifa ya Argentina lakini pia Copa del rey na klabu yake ya FC Barcelona. Na amemaliza kinara wa ufungaji na Assist kwenye La Liga na Copa America.

Wachezaji wengine wanaopewa nafasi ni Jorginho wa Italia na klabu ya Chelsea, Ngolo Kante wa Ufaransa na Chelsea, Cristiano Ronaldo wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno, Robert Lewandowski wa BayernMunich, Marco Verratti wa PSG na Italia, Kelvin de Bruyne wa Mancheater City Ubeligiji, Romelu Lukaku wa Inter Milan na Ubeligiji mchezaji mwingine ni nahodha wa timu ya Taifa ya England Harry Kane.

5. Ni muda wa mkataba aliosaini kiungo wa kimataifa wa Argentina Rodrigo de Paul wa kujiunga na mabingwa wa Hispania Atletico Madrid akitokea Udinese mpaka mwaka 2026, kwa ada ya uhamisho ya Euro milion 36. Ambapo inaripotiwa kuwa kocha wa Atletico Diego Simeone alimpigia Simu yeye binafsi kumshawishi ajiunge na kikosi hicho.

Mchezaji huyo alikuwa na kiwango bora kwenye michuano ya Copa America akiisaidia Argentina kutwaa ubingwa wa kwanza wa Copa America tangu mwaka 1993 na pasi ya bao la ubingwa ilitoka kwake kwenda kwa mfungaji Angel Dimaria. Msimu uliopita alicheza michezo 38 akiwa na Udinese na alifunga mabao 9 na Assist 7.

4. Ni jumla ya mataji ya Ligi kuu soka Tanzania bara aliyoshinda Haruna Niyonzima akiwa na kikosi cha Yanga kati ya msimu wa 2011- 12 mpaka 2016 - 2017. Kabla ya kuondoka klabu hapo na kulijiunga na Simba SC, baadae akarudi kwao Rwanda katika klabu ya AS Kigali na January 2019 akarejea tena Yanga.

Na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba klabu ya Yanga itamuaga mchezaji huyo kwenye mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Ihefu utakao chezwa Julai 15 katika Dimba la Benjamin Mkapa.

3. Ni masaa yaliyotumika kukamilisha upasuaji wa kifundo cha mguu cha bondia Conor McGregor raia wa Ireland.

McGregor alivunjika roundi ya kwanza kwenye pambano ambalo lilikuwa sio la ubingwa dhidi ya Dustin Poirier wa Marekani na pambano hilo likamalizika kwa Dustin kushinda kwa TKO na kwa mujibu wa taarifa, McGregor atakuwa nje ya uringo kwa muda wa wiki sita na atarejea pale atakapo pona jeraha hilo.

2. Ni idadi ya mataji ya Ligi kuu ya Wanawake Tanzania bara waliotwaa klabu ya Simba Queens, ambapo kikosi hicho kitakabidhiwa kombe la ubingwa wa Ligi hiyo msimu wa 2020-21 leo katika dimba la Uhuru ambapo kikosi hicho kitacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Twiga Stars.

Simba Queens walitwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi ya Wanawake msimu wa 2019-20 na wamefanikiwa kuutetea kwa msimu wa 2020-21.

1. Ni nafasi wanayoshikilia klabu ya Simba kwenye msimamo wa VPL na tayari ndio mabingwa wa VPL msimu huu, sasa katika harakati za kuhakikisha wanatetea ubingwa wao kwa msimu wa tano mfululizo kuelekea msimu ujao, mmoja ya wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo Zacharia Hans Poppe amesema mpaka sasa kuna wachezaji 11 wakigeni wanaotaka kujiunga na kikosi chao huku akisistiza kuwa "Kwasasa wachezaji wengi wanataka kuja Simba, nakuhakikishia hakuna mchezaji tutakayemhitaji wa nje tukimtaka tutamkosa, labda wa hapa nyumbani".