Simba yapata 'Jembe' jingine

Friday , 14th Jul , 2017

Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imemtua Dr. Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu hiyo baada ya kamati hiyo kukaa kikao jana jioni.

katibu Mkuu wa Simba SC, Dr. Arnold Kashembe.

Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Kaimu wa rais klabu hiyo, Salim Abdallah na kusema uteuzi wa Katibu Mkuu huyo mwenye shahada ya uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani ulaya  unaanza kufanya kazi mara moja.

Pamoja na hayo, Salim amewataka wanachama na mashabiki wa wekundu wa Msimbazi kuendelea kuwa na utulivu,hususani kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wao wakiwa kwenye shauri lao,liliopo Mahakamani dhidi ya mashtaka yanayowakabili.

 

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi