Ijumaa , 17th Sep , 2021

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC kinarejea jijini Dar es salaam leo Saa 2:00 Usiku kikitokea mkoani Arusha kwa ndege, ambapo kilikuwa kimeweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano wa 2021-22.

Wachezaji wa Simba SC

Simba iliondoka Dar es salaam Septemba 5 kwenda Arusha baada ya kurejea nchini Agosti 29 kutokea nchini Morocco ambako iliweka kambi ya takribai wiki mbili za Pre-season. Wekundu hao wa msimbazi wanarejea ikiwa imebaki siku moja kabla ya tamasha la Simba day litakalofanyika Septemmba 19 katika Dimba la Benjamini Mkapa Dar es salaam.

Katika tamasha hilo la Simba day, Simba itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe mabingwa mara tano (5) wa klabu bingwa Afrika kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na timu hiyo itawasili nchini kesho Jumamosi tayari kwa mchezo huo.