Jumanne , 12th Oct , 2021

Klabu ya Yanga imepigwa faini zaidi ya shilingi milioni 11 na Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa kuvunja baadhi ya sheria na taratibu za mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria Septemba 12, 2021.

Winga wa Yanga, Jesus Moloko akijaribu kumtoka mchezaji wa Rivers united.

Adhabu hiyo imetolewa na kamati ya nidhamu ya CAF kutokana na malalamiko ya Rivers United juu ya baadhi ya viongozi wao kughasiwa na maafisa wa usala,a wa Yanga na baadhi ya mashabiki kuingia uwanjani wakati mchezo huo ambao ulipaswa kuchezwa bila mashabiki.

Taarifa ya kamati hiyo imeeleza kuwa Yanga hawakutoa utetezi wowote juu ya malalamiko hayo na kamati hiyo imewapiga faini ya dolla za kimarekani 5,000 sawa na 11,525, 000 kutokana na matukio hayo.

Kamati hiyo imeenda mbali zaidi na kutoa onyo kali kwa TFF kuwa makini kwa michezo ya ngazi ya klabu na timu za taifa kutokana na timu nyingine za kigeni kulalamikia vipimo vya Uviko 19, kupitiliza kwa idadi ya mashabiki kuingia uwanjani na malalamiko kwenye vyumba kwa kubadilishia nguo.