Rasmi! Yanga na Azam kucheza bila mashabiki CAF

Jumamosi , 11th Sep , 2021

Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limeiliekeleza shirikisho la Soka nchini kuwa michezo ya hatua ya mtoano ya awali ya michuano hiyo ichewzwe bila ya mashabiki ikiwa ni muendelezo wa juhudi za shirikisho hilo kujikinga dhidi ya Covid-19.

Mashabiki wa klabu ya Yanga wakiwa kwenye dimba la BW Mkapa kushangilia timu yao kwenye moja ya mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara.

Taarifa hiyo sasa inaelekeza ni rasmi wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kimataifa yaani mchezo wa saa 1:00 usiku wa leo wa Azan dhidi ya Horseed ya Somalia utakaochezwa leo Septemba 11, 2021 kwenye dimba la Chamazi na ule wa Yanga dhidi ya Rivers United wa kuwania makundi Klabu bingwa Afrika utakaochezwa saa 11:00 jioni ya kesho Septemba 12, 2021 kwenye dimba la BW Mkapa itachezwa bila mashabiki.

Taarifa ya TFF imeeleza kuwa;

Uwezekano wa wawakilishi hao kucheza na watazamaji wao utategemeana na juhudi zao za kuishawishi CAF iwaruhusu kwenye michezo ijayo.