Jumatatu , 15th Feb , 2016

Meneja wa Leicester City Claudio Ranieri anaamini uamuzi wa mwamuzi Martin Atkinson kumtoa Danny Simpson kwa kadi nyekundu katika mechi ya jana waliyopoteza dhidi ya Arsenal kwa bao 2-1 ndio uliosababisha mazingira magumu sana kwa timu yake.

Kocha wa klabu ya Leicester City Claudio Ranieli

Meneja huyo anaamini timu yake ingeshinda mechi hiyo katika uwanja wa Emirates kama wangecheza wachezaji 11 hadi dakika ya mwisho.

Ranieli amesema mechi hiyo ilikuwa ya kasi na rafu nyingi hivyo anaamini mwamuzi alipaswa kuwa na busara kwa kutotoa kadi zilizoharibu mchezo.

Jamie Vardy aliwapatia Mbweha hao goli la kuongoza kabla ya mapumziko kwa mkwaju wa penalt kabla ya Arsenal kurejea kwa nguvu na kupata ushindi wa mabao kutoka kwa Theo Walcott na Danny Welbeck baada ya Leicester kupungua hadi watu 10 mnamo dakika ya 54 kufuatia kutolewa kwa Simpson.

Kwa upande wa kocha wa Arsenal Mfaransa Arsenal Wenger amesema ushindi huo umewajenga kisaikolojia na sasa anaamini wachezaji wake watakuwa na morali ya kuendelea kupambania ubingwa.

Arsenal wamefikisha pointi 51 sawa na Totenham Hotspurs lakini wakizidiwa kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.