Ijumaa , 20th Mei , 2022

Polisi wa jiji la Merseyside wameanza kufanya uchunguzi juu ya taharuki iliyozuka kwenye uwanja wa Goodson Park inayomuhisisha shabiki wa Everton dhidi ya Kocha Mkuu wa Crystal Palace, Patrick Vieira.

Picha za video zinaonyesha vieira akimpiga teke shabiki wa Everton baada ya mchezo huo kumalizika.

Tukio hilo lilitokea baada ya Mashabiki wa Everton kuingia uwanjani baada ya dakika tisini za mchezo huo ambao wenyeji Everton waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Crystal Palace mchezo ambao Everton walitoka nyuma kwa mabao 2-0 na kujihakikishia nafasi ya kucheza  EPL msimu ujao.

Uchunguzi huo umeanza kufanyika baada ya picha za video kuonesha Shabiki wa Everton akimdhihaki Vieira aliyeshindwa kuvumilia dhihaka hizo jambo lililopelekea Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal kumpiga teke Shabiki huyo.

Polisi wa Merseyside wameanza kutafuta kanda mbalimbali za video za CCTV ilikujilidhisha na uchunguzi wao huku Vilabu vya Everton na Crystal Pace vikiwa bado havijatoa kauli yoyote juu ya tukio hilo.