Jumatano , 3rd Aug , 2022

Taarifa kutoka Turin nchini Italia zinasema kiungo wa Juventus raia wa Ufaransa Paul Labile Pogba amekataa kufanyiwa upasuaji kwenye goti lake lililojeruhiwa, na badala yake amechagua kufanyiwa matibabu ya kawaida bila kupasuliwa.

Paul Pogba

Pogba amefanya uamuzi huo ili apate nafasi ya kushiiriki michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu nchini Qatar, kwani endapo atakubali kufanyiwa upasuaji basi atalazimika kukaa nje kwa zaidi ya miezi minne kitendo ambacho kitamfanya ashindwe kushirikishi michuano hiyo mikubwa ya soka Duniani.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 29 anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kisichopungua wiki tano kama matibabu yataenda vizuri vile inavyotarajiwa, lakini endapo hali ikiwa tofauti basi huenda akakosekana kwa kipindi kirefu zaidi ya hapo.

Pogba alipata jeraha hilo la goti ikiwa ni wiki tatu tu tangu ajiunge tena kwa mara ya pili na Kibibi kizee hicho cha Turin (Juventus) kwa mkataba wa maika minne akitokea Manchester united alipodumu kwa kipindi cha miaka 6 akiwa amejiunga kwa mara ya pili na mashetani hao wekundu akitokea Juventus aliporejea hivi sasa.