Nyota chipukizi 25 wanaowania tuzo Ulaya

Tuesday , 19th Sep , 2017

Jumla ya nyota chipukizi 25 wa soka barani Ulaya wametangazwa leo kuwania tuzo ya Europe Golden Boy 2017 ambapo majina kama Rashford, Mbappe na Dembele yameonekana kuongoza orodha hiyo.

Tuzo ya Europe Golden Boy hutambua kijana mwenye kipaji zaidi cha soka barani Ulaya chini ya umri wa miaka 21 ambapo mwaka huu kumekuwepo na ongezeko kubwa la vijana wenye vipaji vya hali ya juu.

Kylian Mbappe ambaye alifanya vizuri msimu uliopita akiwa na Monaco msimu huu amehamia PSG na Ousimane Dembele alifanya vizuri msimu uliopita akiwa na Borrusia Dortmund kabla ya kuhamia Barcelona ndio wanatajwa sana huenda wakatwaa tuzo hiyo ambayo itatolewa mwezi Oktoba.

Tuzo hizo huandaliwa na gazeti la Tuttosport  la Italia kisha kupigiwa kura na waandishi wa habari za michezo barani Ulaya.

Orodha kamili

Aaron Martin (Espanyol), Jean-Kevin Augustin (RB Leipzig), Rodrigo Bentacur (Juventus), Steven Bergwijn (PSV), Dominic Calvert-Lewin (Everton), Federico Chiesa (Fiorentina), Ousmane Dembele (Barcelona), Amadou Diawara (Napoli), Kasper Dolberg (Ajax), Gianluigi Donnarumma (AC Milan), Gabriel Jesus (Manchester City), Joe Gomez (Liverpool), Benjamin Henrichs (Bayer Leverkusen), Borja Mayoral (Real Madrid), Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain), Emre Mor (Celta Vigo), Reece Oxford (Borussia Monchengladbach), Christian Pulisic (Borussia Dortmund), Marcus Rashford (Manchester United), Allan Saint-Maximim (Nice), Dominic Solanke (Liverpool), Theo Hernandez (Real Madrid), Youri Tielemans (Monaco), Enes Unal (Villarreal), Kyle Walker-Peters (Tottenham).