Jumatano , 30th Mar , 2022

Bingwa mara 4 wa Grand Slam upande wa wanawake Naomi Osaka amefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya wazi ya Miami baada ya kushinda seti mbili mfululizo dhidi ya Danielle Collins raia wa Marekani.

Naomi Osaka

Osoka raia wa Japani na mchezaji namba moja wa zamani kwenye viwango vya ubora ameshinda kwa 6-2, 6-1 kwenye mchezo uliochezwa kwa muda wa Saa 1. Lakini pia muda mwingi wa mchezo huo Danielle Collins alicheza akiwa na maumivu ya kifundo cha mguu.

Katika hatua ya nusu fainali Osoka atacheza dhidi ya Belinda Bencic wa Switzerland, Belinda amefuzu hatua hii baada ya kumnyuka Daria Saville wa Australia kwa seti 6-1 6-2. Mchezo huu wa nusu fainali kati ya Naomi Osaka na Belinda Bencic unachezwa kesho Machi 31.