Jumatano , 13th Oct , 2021

Mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop amekutwa amefariki ndani ya nyumba yake eneo la Iten, Elgeyo, Kaunti ya Marakwet nchini Kenya leo Oktoba 13, 2021.

Mwanariadha wa Kenya Agnes Tirop enzi za uhai wake

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Agnes mwenye miaka 25, amekutwa na majeraha ya kuchomwa na kitu tumboni kwake.

Agnes aliiwakilisha Kenya kwenye michuano ya Olimpiki ya Tokyo mapema mwaka huu katika mbio za mita 5,000 na kushika nafasi ya 4.

Amewahi kushirikia mashindano mbalimbali na kushinda ikiwemo mwaka 2005 alipoibuka mshindi wa ubingwa wa dunia kwa wanariadha (World Cross Country Championships)

Pia mwaka 2017 na 2019 alishinda ubingwa wa dunia wa riadha maarufu kama World Championships.