Jumatano , 11th Mei , 2022

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Wallace Karia amefanya mkutano na Uongozi wa Mkoa wa Arusha juu ya maandalizi ya kufanyika kwa mkutano mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF.

(Rais wa TFF Wallace Karia)

Mkutano huo utafanyika mkoani Arusha hapa nchini Tanzania ifikapo mwezi wa nane mwaka huu, huku viongozi wa mashirikisho ya mpira wa miguu Afrika wakitajwa kuhudhuria mkutano huo. Wachezaji wa zamani wa mpira wa miguu Afrika pamoja na Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Duniani (FIFA) Gianni Infantino pia anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.

Kufuatia jambo hilo Rais Karia amesema watatumia fursa hiyo kufanya utalii wa kimichezo pamoja na utalii wa kimikutano lengo likiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii wa ndani huku Serikali ya mkoa wa Arusha ikiwa katika hali nzuri ya maandalizi ya tukio hilo.