Jumanne , 13th Feb , 2018

Kiungo wa klabu ya Hull City ya England Ryan Mason, amelazimika kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 26 kwa tatizo la jeraha la fuvu la kichwa alilopata kwenye mechi dhidi ya Chelsea.

Mason amechukua uamuzi huo wa kustaafu baada ya kupewa ushauri wa madaktari wa upasuaji wa kichwa aliofanyiwa katika hospitali ya St. Mary mjini London, ambapo madaktari wameeleza kuwa Mason kuwa hai hadi sasa imekuwa ni bahati tu.

Katika mchezo huo wa EPL katika uwanja wa Stamford Bridge Januari 2016, Mason aligongana kichwa kwa kichwa na beki wa Chelsea Gary Cahill na kupasuka ambapo alitibiwa kwa dakika nane uwanjani kabla ya kukimbizwa Hospitali.

Baada ya kutibiwa Mason alianza mazoezi na klabu hiyo tena Mei 2017 lakini hakupata nafuu zaidi ya kucheza tena ambapo alikutana na watalaam zaidi wakamshauri aachane na soka.

Klabu ya hull City imewashukuru wale wote waliomsaidia kupona katika kipindi cha miezi 12 ya kuumwa kwake na sasa Mason anaanza maisha mapya nje ya soka. Mason ambaye ni raia wa England alianzia soka kwenye klabu ya Tottenham Hotspurs.