Jumanne , 23rd Nov , 2021

Inaripotiwa kuwa klabu ya Manchester United ipo kwenye mazungumzo na kocha wa PSG Mauricio Pochettino ikiwa inamtaka aje kuchukua nafasi iliyoachwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer aliyefutwa kazi siku ya Jumapili. Na Zinedine Zidane anatajwa kuchukua nafasi ya Pochetino kama ataondoka PSG.

Mauricio Pochettino

Inadaiwa kuwa Pochetino hana mahusiano mazuri na Mkurugenzi wa ufundi wa PSG Leonardo na hiyo ndio sababu inayotajwa inaweza kumfanya kocha huyo raia wa Argentina kuondoka kwenye kikosi hicho cha matajiri wa jiji la Paris nchini Ufaransa.

Mkataba wa sasa wa Pochetino na PSG unamalizika mwaka 2023 na kwa timu itakayovunja mkataba huo itapaswa kulipa Pauni million 10, ambayo ni zaidi ya bilioni 30 kwa pesa za kitanzania kama fidia. Kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zadane anapigiwa upatu kuwa kocha mpya wa PSG endapo Kama Pochetino akikubali kujiunga na Manchester United.

Katika ripoti mbalimbali zinataja kuwa Pochetino ndio kocha chaguo la kwanza la Manchester United katika orodha ya makacho wanaohusishwa kujiunga na timu, makocha wengine ni Zinedine Zidane, na Brendan Rodgers wa Leicester City