Alhamisi , 15th Jul , 2021

Baada ya ofa ya Manchester City ya pauni million 100 ya kumsaji Harry Kane kukataliwa na Tottenham sasa klabu hiyo inajipanga kuhamishia nguvu kwa mshambuliaji wa Bayern Munich Roberto Lewandowski.

Roberto Lewandowski

Manchester City wapo sokoni kutafuta mshambuliaji wa daraja la juu ambaye atachukua nafasi iliyoachwa na Sergio Kun Aguero ambaye amejiunga na FC Barcelona baada ya kumaliza mkataba. Harry Kane wa Tottenham na Erling Haaland wa Dortmund ndio wachezaji wanaotajwa kuwa wanawaniwa kwa ukaribu na Man City.

Mabingwa hao watetetzi wa EPL inaripotiwa kuwa ofa yao ya ada ya uhamisho ya Pauni million 100 zaidi ya billion 321 kwa pesa za kitanznaia kwa ajili ya kumsajili Kane ilikataliwa na Tottenham ambao nao wameweka wazi kuwa bado wanahitaji huduma ya mshambuliaji huyo ambae kabakiza mkataba wa miaka miwili, wakati kwa Haaland dau la Pauni million 175 zaidi ya bilioni 562 linalotajwa kama ada ya uhamisho ya mshambuliaji huyo kinda, City hawapo tayari kulipa dau hilo.

Sasa baada ya kuonekana kuna ugumu kwenye kumpata mmoja kati ya washambuliaji hao, inatajwa Man City wameanza kufuatilia mkataba wa Roberto Lewandowski na kuona kama itawezekana kumsajili mshambuliaji huyo raia wa Poland mwenye umri wa miaka 32.

Lewandowski amebakiza mkataba wa miaka miwili na Bayern Munich, na aliwahi kufanya kazi na kocha wa Man City Pep Guardiolandani ya kikosi hicho cha The Bavarians kati ya mwaka 2014 hadi 2016 na hiyo inatajwa kuwa inaweza kuwa sababu ya kumshawishi mshambuliaji huyo.

Msimu uliopita alifungwa mabao 48 kwenye mashindano yote huku mabao 41 kati ya hayo yakiwa ni ya Ligi Kuu na ni rekodi kwenye ligi hiyo kwa mchezaji kufunga idadi hiyo ya mabao kwenye msimu mmoja.