Ijumaa , 14th Mei , 2021

Klabu ya Liverpool imerejesha matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi kuu England, baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Manchster United jana Usiku na sasa kikosi hicho kimefikisha alama 60 ikiwa ni tofauti ya alama 4 na na Chelsea iliyo nafasi ya nne.

Wachezaji wa liverpool wakishangilia bao kwenye mchezo dhidi ya Manchester United jana Usiku katika dimba la Old Traford

Mabao ya ushindi ya Liverpool yalifunga wa Roberto Firmino aliyefunga mara mbili, Diogo Joto na Mo Salah wakati yale ya Manchester United yalifungwa na Bruno Fernandez na Marcus Rashford.

Ushindi huo umeifanya Liverpool ifikishe alama 60 na imepanda mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo kutoka nafasi ya sita, ikiwa ni tofauti ya alama nne dhidi ya Chelsea inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo nafasi ambayo inatoa tiketi ya kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya, lakini pia kikosi hicho kinafaida ya kuwa na mchezo mmoja mkononi, wamecheza michezo 35 wakati Chelsea na Leicester City zimecheza michezo 36.

Na endapo kama Liverpool ikishinda mchezo wake unaofata dhidi ya West Bromwich Albion Mei 16, 2021. itafikisha alama 63 na tofauti yao na Chelsea itakuwa alama moja na watakuwa na idadi sawa ya michezo, Chelsea haitacheza mchezo wa Ligi Kuu mwishoni mwa wiki hii kwani itakuwa ikicheza mchezo wa fainali ya kombe la FA Cup dhidi ya Leicester City.