Jumanne , 19th Sep , 2017

Shirikisho la soka Tanzania TFF leo  limetangaza tarehe ya kuanza kwa michuano ya Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL) ambayo ni Septemba 30, mwaka huu.

Tarehe hiyo ya kuanza kwa SDL imeambatana na ratiba ya michezo ya ufunguzi ambapo kutakuwa na michezo ya kundi A kati ya Abajalo na Cosmopolitan, Namungo na Reha huku kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini. Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkina Faso na Ihefu wakati Boma itacheza na Mkamba Rangers na Kundi D zitacheza Bulyanhulu na Milambo.

Katika Kundi hilo la D mchezo kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye uwanja huo huo.

Sababu za mabadiliko haya ni kutokana na mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe 30.09.2017 katika uwanja huo. Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ifanye mabadiliko.