Ijumaa , 15th Jan , 2016

Jumamosi hii klabu ya Manchester City na Leicester City zina nafasi murua ya kutwaa uongozi wa Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa watafanya vyema kwenye Mechi zao kwa kuwa Vinara Arsenal wao wanacheza Jumapili.

Ligi kuu ya soka nchini Uingereza

Arsenal na Leicester City zote zipa Pointi 43 lakini Arsenal wako juu kwa ubora wa Magoli wakati Manchester City wako Nafasi ya 3 wakiwa na Pointi 40.

Kesho Manchester City ambao Jumatano walitoka sare ya 0-0 na Everton, wako kwao Etihad kucheza na Crystal Palace na Leicester City waloiachapa Tottenham bao1-0 Siku ya Jumatano, wako Ugenini Villa Park kucheza na Aston Villa.

Sare au ushindi kwa Leicester utawaweka Leicester kileleni lakini wakifungwa na City kushinda basi City watatwaa uongozi pengine hadi Jumapili ambapo ushindi kwa Arsenal, wakiwa Ugenini dhidi ya Timu ngumu Stoke City, utawarejeshea Arsenal uongozi wao wa Ligi.

Mbali ya Mechi hii ya Arsenal, Jumapili pia ipo Bigi Mechi ya Mahasimu wakuu huko Uingereza kati ya Liverpool na Man United, Klabu ambazo zina Masapota wengi huko na pia zenye mafanikio makubwa kupita zozote Nchini humo.

Kama ilivyo kwa Sare ya Liverpool ya bao 3-3, Manchester United nao walitoka sare ya bao 3-3 na Newcastle huko Saint James Park Siku ya Jumane.

Kimsimamo, Man United wako Nafasi ya 6 wakiwa na Pointi 34 na Liverpool ni wa 9 wakiwa na Pointi 31.

Katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Msimu huu iliyochezwa huko Old Trafford, Man United waliitwanga Liverpool 3-1 hapo Septemba 12 kwa Bao za Blind, Herera na Martial, ambae alikuwa akicheza Mechi yake ya kwanza kabisa, wakati lile la Liverpool lilifungwa na Benteke.

Ratiba ya mechi za ligi kuu nchini Uingereza
Jumamosi
1545 Tottenham v Sunderland
1800 Bournemouth v Norwich
1800 Chelsea v Everton
1800 Man City v Crystal Palace
1800 Newcastle v West Ham
1800 Southampton v West Brom
2030 Aston Villa v Leicester
Jumapili Januari 17
1705 Liverpool v Man United
1915 Stoke v Arsenal
Jumatatu Januari 18
2300 Swansea v Watford