Kwa Gyan, Simba kulamba dume!

Saturday , 15th Jul , 2017

Endapo Simba itafanikiwa kunasa saini ya straika mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan itakuwa imelamba dume kutokana na ubora wa mchezaji huyo.

Nicholas Gyan

Taarifa zinasema kuwa Gyan ambaye ni mdogo wa Asamoah Gyan, nyota na nahodha wa timu ya Taifa ya Ghana ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchi hiyo msimu uliomalizika hivi karibuni ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 19 ambao kwa wachezaji ndio umri wa kuonyesha makali yao.

Taarifa zinaendelea kudodosa kuwa straika huyo alitarajiwa kutua nchini kati ya jana usiku na leo akiwa sambamba na Kaimu Makamu wa Rais , Iddi Kajuna, ambaye alikwenda Ghana kukamilisha usajili wa straika huyo kinda.

Recent Posts

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Current Affairs
CCM yatoa kauli yake kuhusu kifo cha mwanafunzi