Alhamisi , 17th Nov , 2022

Kikosi cha KMC kimeanza maandalizi kuelekea katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Singida Big Star utakaochezwa Novemba 23 katika Uwanja wa Liti Mkoani Singida.

Kikosi cha KMC

Kikosi hicho cha Manispaa ya Kinondoni kimeanza maandalizi yake leo mara baada ya kutoka kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Dodoma Jiji kwa magoli mawili kwa moja.

Katika maandalizi hayo, Kocha Mkuu Thierry Hitimana amepanga programu mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho ya makosa mbalimbali  yaliyojitokeza kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji na hivyo kupelekea kupoteza ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

KMC FC inajipanga kufanya vizuri kwenye mchezo unaokuja licha ya kuwa itakuwa ugenini na kwamba pamoja na ushindani uliopo kwenye Ligi bado Timu ipoimara katika kuhakikisha kuwa inafanya vizuri kwenye michezo inayokuja.

"Tunakwenda kwenye mchezo mwingine mgumu na wenye ushindani ambao  tutakuwa ugenini, bado hatujapata matokeo mazuri kwenye michezo minne  tuliyocheza ambapo kati ya hiyo tumepata amala moja dhidi ya Geita, ila hatukati tamaa kwasababu tunakikosi bora.

"Mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji tulipoteza kutokana na changamoto ya uchovu, nanimatokeo ambayo yalimuumiza kila mmoja, lakini kama Timu bado tupo imara na hatujakata tamaa kwasababu tunafahamu wachezaji wetu wapo kwenye kiwango kizuri .

Mashabiki zetu na watanzania wote ambao mnatuunga mkono sikuzote tunawasihi msiwe na hofu pamoja na kwamba hatuna matokeo mazuri kwenye michezo minne mfululizo lakini bado tunanafasi nyingine ya kufanya vizuri kwenye michezo inayokuja.

Kwa upande wa Afya za wachezaji wote wako vizuri, lakini Matheo Anton anaendelea na programu ya mazoezi mepesi ya peke yake, Awesu Ally Awesu bado hajajiunga na wenzake na hivyo anaendelea na matibabu pamoja na uangalizi wa Daktari.