Alhamisi , 17th Jun , 2021

Uongozi wa Fountain Gate Academy umemtambulisha Denis Kitambi kuwa kocha wao mpya kwa msimu ujao wa daraja la kwanza kuchukua nafasi ya Mohamed Muya.

Kocha Denis Kitambi

Kitambi ambaye ni kocha msaidizi wa zamani wa timu ya Simba na pia aliwahi kufanya kazi Ndanda, FC Azam na AFC Leopards ya Kenya, amesaini kandarasi ya msimu moj akiwa na jukumu kubwa la kuipandisha Ligi kuu timu hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa timu hiyo yenye makao makuu yake mjini Dodoma Japhat Makau ,amekuwa na maono ya kuona timu aliyoianzisha kutokana na jumuiya ya wanafunzi wa shule ‘Academy’ anafanikiwa kupanda daraja hadi ligi kuu.

Katika msimu uliomalizika wa daraja la kwanza, Fountain Gate Academy walilazimika kucheza hatua ya mtoano ’play off’dhidi ya Lipuli kujinusuru kushuka daraja la pili.

Kitambi ni kocha Mtanzania kijana ambaye pia ni msomi mwenye uzoefu mkubwa kwa sasa akiwa amefanya kazi kitaifa na kimataifa ,amepata uzoefu mkubwa kwa kufanya kazi chini ya makocha wakubwa kama Stewart Hall, Patrick Aussems nk anarekodi ya kuipandisha Ndanda ligi kuu mwaka 201