Jumanne , 16th Aug , 2022

Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Wallace Karia amefafanua picha ambayo imekuwa ikisambaa mitandaoni ikimuonesha akiwa amevaa jezi ya klabu ya Simba 

Karia amesema ni kweli alivaa jezi hiyo na ni tukio la miaka mingi tofauti na inavyoelezwa mitandaoni
"Lile ni tukio la miaka mingi sana wakati bado ni makamu, niliagizwa na Rais wangu Malinzi niende nikamuwakilishe kwenye Simba day, nilivyofika na fulana yangu ya Blue wakanipa jezi, tukio la watu huwezi kuliharibu kwa kukataa jezi, Jezi kuvaa na moyo wa mtu ni tofauti, kuna watu hawavai Jezi lakini wanafanya mambo ya ajabu" amesema Karia

Aidha Karia amesema yeye sio mwanachama wa Simba kama inavyoelezwa bali yeye ni mwanachama wa Coastal Union na amekuwa pia kiongozi wa timu hiyo