Alhamisi , 24th Mei , 2018

Baada ya kuitumikia Barcelona kwa muda mrefu  tokea akiwa kinda, Andres Iniesta leo hii ametangaza kujiunga na klabu ya Vissel Kobe ya nchini Japan kwa muda wa miaka miwili.

Iniesta amekua nahodha wa Barcelona tangu mwaka 2015 na mwaka jana alisaini mkataba wa maisha kuitumikia klabu hiyo.

Iniesta alitangaza kwamba angeondoka katika klabu ya Barcelona baada ya msimu wa ligi kuu ya Hispania kumalizika baada ya misimu 16 ndani ya Catalunya. 

Timu hiyo ya Vissel Kobe katika ligi ya J-League ipo katika nafasi ya 6 baada ya michezo 15, ilimsajili Lucas Podolski mwaka uliopita lakini mshambuliaji huyo atakua nje mpaka mwishoni mwa mwezi Juni baaada ya kupata majeraha.  

Mkurugenzi Mkuu wa Wadhamini wakuu wa Barcelona, Mikitan amesema kuwa hakuna asiyefahamu kuwa Iniesta kaitumikia klabu hiy kwa mafanikio na kumtakia kila la kheri mchezaji huyo

‘Iniesta ni mchezaji wa dunia, wengi wetu wanakumbuka goli lake alilofunga katika michuano ya Dunia Afrika Kusini ambalo liliiletea Hispania Kombe hilo kwa mara ya kwanza”, amesema Mikitan