Imewezekana kwa Neymar, hata Messi itawezekana!

Saturday , 12th Aug , 2017

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anaamini kuwa rekodi ya uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona kwenda Paris Saint-Germain inafanya kuwezekana kulipwa kwa Euro milioni 300 zinazohitajika ili kuvunja mkataba wa Lionel Messi.

Klopp anasema kitendo cha Paris-Saint Germain kuridhia kuvunja mkataba wa Neymar na Barcelona, ni onyo kwa miamba hiyo ya Camp Nou kuwa hata kwa Messi inawezekana mkataba wake kuvunjwa licha ya kwamba zitahitajika Euro milioni 300.

PSG iliipiku rekodi ya hivi karibuni iliyolipwa na Manchester United kwa Paul Pogba mwaka uliopita kwa kukubali kulipa Euro milioni 222 ili kumnasa Mbrazil huyo kutoka Barca.

Klopp anaamini kuna klabu inaweza ikalipa zaidi ya dau hili ili kuipata huduma ya Messi, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Dunia 'Ballon d'Or' mara tano.