Jumatatu , 10th Mei , 2021

Kocha mzoefu Sam Allardyce kwa mara ya kwanza katika historia yake ameshusha timu daraja, kutoka ligi kuu ya Uingereza kwenda Championship kwa msimu 2021/2022.

Kocha Mzoefu Sam Allardyce

Kichapo 3-1 kutoka kwa Arsenal, kilikamilisha safari yake ya kuungana na Sheffield United kushuka daraja kutokana na alama walizonazo (26), katika michezo 35 waliyocheza ikiwa na maana wamebakiza michezo 3 tu, huku timu ya nne kutoka mwisho ikiwa na alama 36 ambayo ni Burnley ambazo haziwezi kufikiwa na timu yeyote kati ya tatu zilizo chini yake.

Sam Allardyce maarufu kama Big Sam, kocha aliyevifundisha vilabu kadhaa ikiwemo timu ya taifa ya Uingereza maarufu kama 'Three lions' amekuwa na sifa ya kuvinusuru vilabu mbalimbali katika janga la kushuka daraja.

'Big Sam' alijiunga na West Bromwich Albion 16/12/2020 kuchukua nafasi ya Slaven Billic aliyetimuliwa na timu hiyo baada ya mwenendo mbaya wa matokeo.

Takwimu za Sam Allardyce katika EPL, ameongoza timu kwa misimu 17 jumla ya michezo 534 ameshinda 178 sare 145 na kupoteza 211 , agoli ya kufunga 628 na magoli ya kufugwa 740 akiwa na timu tofauti tofauti za madaraja ya kati kama Everton, Crystal,Westham na West Bromwich Albion.