Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia moja ya bao walilofunga dhidi ya Northen Macedonia.
Magoli mawili ya mshambuliaji Timo Werner, Kai Havertz na Jamal Musiala yametosha kuwapa nafasi Ujerumani tiketi ya kushiriki michuano hiyo mikubwa duniani baada ya kufikisha alama 21 huku akisaliwa na michezo miwili dhidi ya Liechtenstein nyumbani mwezi November na ugenini dhidi ya Armenia.
Baada ya kuwavusha Ujerumani, Kocha Hansi Flick atakuwa na kibarua pevu cha kusaka mafanikio zaidi kwa taifa hilo baada ya miaka 15 ya mtangulizi wake Joachim Low kuwapa kombe la dunia mwaka 2014 nchini brazil na kombe la mabara mwaka 2017 nchini Urusi.
Hii itakuwa mara ya 20 kwa taifa la Ujerumani kushiriki kombe la dunia wakiwa nyuma ya Brazil ambao wameshiriki mara 21 huku Ujerumani wanarudi wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kuondoshwa kwenye hatua za makundi kama bingwa mtetezi mwaka 2018 nchini Urusi.