Jumatatu , 12th Jul , 2021

Mwanamuziki na shabiki wa klabu ya Yanga, G Nako ametumia ukurasa wake wa instagram kumshawishi mchezaji mwandamizi wa klabu ya Simba Jonas Mkude ili ajinge na wana jangwani hao.

Picha ya pamoja Jonas Mkude na G Nako

Kwenye picha ya pamoja ambayo ame-share msanii huyo ameandika “mtu m’ bad Jonas Mkude mwandamizi, Baba jangwani hatuna bayaa mara paap”, huku naye King Kiba akikazia kwa kusema “kabisa G hatuna bayaa”.