Jumapili , 10th Oct , 2021

Tyson Fury amemchapa Deontay Wilder kwa Knock Out (KO) raundi ya 11 na kutetea ubingwa wake wa WBC huku akiwa ndio bondia ambaye hajapoteza pambano. 

Tyson Fury (nyuma) alipompiga ngumi Deontay Wilder (mbele) raundi ya 11 na kumfanya ashindwe kuendelea na pambano.

 

Mpaka sasa Fury raia wa Uingereza mwenye miaka 33, amepigana mara 32, ameshinda 31 na sare 1. Wilder sasa amepigana mara 45, amesinda 42, sare 1 na kupigwa mara 2.

Hili lilikuwa pambano la tatu kukutana kwa mabondia hao ambapo mara ya kwanza walitoka sare mwaka 2018, kabla ya Fury kushinda mwaka 2020 na leo ameshinda pia.