Alhamisi , 16th Sep , 2021

Timu ya taifa ya soka England, imefanikiwa kupanda kwenye viwango vya soka duniani vitolewavyo na shirikisho la soka duniani FIFA leo Septemba 2021.

Kikosi cha timu ya taifa ya England kilichoshiriki michuano ya UEFA EUROS Julai mwaka 2021.

England imepanda kwenye nafasi hiyo baada ya kuwa na mfulululizo wa matokeo ya ushindi kwenye michezo ya kuwania kufuzu kombe la dunia dhidi ya Andorra, Hungary na Poland pamoja na kucheza fainali ya michuano ya EUFA EUROS yaliyomalizikia Julai mwaka huu.

Pia wakisifika kwa kutandaza soka safi, England imefikia rekodi yao waliyoiweka mwaka 2012 kwa kushika nafasi ya tatu kwenye viwango hivyo vya ubora na sasa wamefanikiwa kumpiku bingwa wa dunia, timu ya taifa ya Ufaransa anayoshika nafasi ya nne baada ya kuboronga hivi karibuni.

Ikumbukwe kuwa, Ufaransa ilicheza michezo mitano mfululizo bila kupata ushindi na hatimaye kuibuka na ushindi wa kwenye mchezo wake wasita hivyo kushuka kwenye nafasi moja. Kwa upande mwingine, timu ya taifa ya Ubeligiji imeendelea kung'ang'ania nafasi ya kwanza kwa mwaka wa saba mfululizo.