Alhamisi , 8th Sep , 2016

Chama cha Mpira wa Pete Tanzania, CHANETA, kimekumbusha vyama vya mikoa, kupeleka majina ya mabingwa wao kabla ya Oktoba 10, mwaka huu, kwa ajili ya ligi daraja la pili, itakayofanyika Dodoma, Oktoba 22.

Wachezaji wa Netball

Mwenyekiti wa CHANETA, Anna Kibira, amesema kuwahisha kupeleka mabingwa hao, kutarahisisha maandilizi ya kwenda vizuri.

Mikoa yote ya Tanzania Bara, inatarajiwa kupeleka mabingwa wao kwa ajili ya kupata bingwa wa ligi daraja la pili taifa, 2016.