
(Nyota wa tennis Victoria Azarenka )
Azarenka mwenye umri wa miaka 32 ambaye alitwaa ubingwa wa Australian Open mwaka 2012 na 2013 alipoteza kwa seti 6-2 na 3-0 huku hii ikiwa ni mara ya pili kwa nyota huyo kuchukua mapumziko kama ilivyokuwa msimu 2016/17 baada ya kutengana na mzazi mwenzie kisha kurejea tena kwenye tennis mwaka 2018.
" wiki mbili zilizopita sikuwa sawa kutokana na matatizo binafsi ya kifamilia ndio maana mchezo uliopita nilitumia muda mwingi kucheza na kushinda lakini kwa sasa nataka kuchukua likizo na nitarejea baadae kidogo” amesema Azarenka
Fruhvirtov sasa atapambana na Mhispania Paula Badosa kwenye hatua ya 16 bora huku akivunja rekodi ya kutinga hatua hiyo kama mchezaji kinda tangu mwaka 2004 huku akikamata nafasi ya 279 kwa viwango vya ubora wa tennis duniani kwa upande wa wanawake