mshambuliaji wa klabu ya soka ya Azam Fc Farid Mussa akishangilia moja bao alilofunga kwenye mechi ya ligi kuu ya soka Tanzania bara
Afisa habari wa klabu hiyo Jaffar Iddy Maganga amesema mpaka sasa si klabu wala Jamal Kasongo ambaye ni wakala wa wachezaji aliyewasiliana na Azam juu ya kuhitajiwa kwa mchezaji huyo.
Jaffa amesema ili kumruhusu nyota wao kwenda huko anakohitajika ni lazima utaratibu ufuatwe ambao ni maombi ya maandishi rasmi ili wao kama Azam wajilidhishe.
Hivi karibuni kulikuwemo taarifa za nyota huyo kuwa huenda angeelekea barani Ulaya kufanya majaribio kucheza soka la kulipwa lakini mpaka sasa hakujawa na taarifa rasmi.

