Katika taarifa yake, Msemaji wa Azam FC, Jaffar Iddi Maganga amesema timu yao inakwenda Mtwara ikiwa na kikosi cha wachezaji 16 kwa mwaliko wa Ndanda FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara pia.
Maganga amesema Azam FC watakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya Ndanda FC itakayohitimisha shamrashamra za Ndanda Day Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Jaffar amewataja wachezaji wanaokwenda safari hiyo kuwa ni Metacha Mnatha, Godfrey Elias, Abdallah Heri, Gadiel Michael, Bryson Rafael, Prosper Joseph, David Mwantika, Mcha Khamiss na Kelvin Friday.
Wengine ni Shaaban Idd, Sadallah Mohamed, Stanislaus Ladislaus, Masoud Abdallah, Optatus Rupekenya, Odas Rajab, Joseph Kauju na benchi la Ufundi, Dennis Kitambi, Iddi Nassor ‘Cheche’, Saleh Jumapili, Twalib Mbarak, John Matambala na Iddi Abubakar.


