
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu ya Azam, Zacharia Thabiti almaarufu 'Zakazakazi'.
Zaka amesema, “Mara zote ambayo Azam FC imeshiriki mashindano haya yalipofanyika nyumbani imefika hatua ya fainali kuanzia mwaka 2012, mashindano yalifanyika hapa na Azam ikafika fainali, mwaka 2015, ikafika hapa na timu ikafika fainali na ikawa mabinga na 2018 ikawa mabingwa na safari hii tena mashindano haya yanafanyika hapa na timu ipo hatua ya nusu fainali”
“Sasa endapo safari itaishia hapa maana yake itakuwa hiki kizazi kilichopo sasa ni kikazi ambacho kimeshindwa kufikia mafanikio ya waliotangulia. Ila cha msingi ni kuhakikisha kwamba ile 'Legacy', ile 'standard' ambayo ilikwishwa wekwa inafikiwa na hiki ni kitu ambacho vijana wetu wataingia kwenye mchezo wa kesho kuhakikisha kinakuwa”.
Zaka amemaliza kwa kujinasibu akisema kuwa, kikosi chao kimeandaliwa vizuri, vijana wana ari kwasababu wanataka kuwa sehemu ya historia na utamaduni huo wa klabu na hata mchezaji Emmanuel Charles atarejea kikosini baada ya kuukosa mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu.
Mshindi wa mchezo kati ya Azam dhidi ya Nyasa Big Bullets atacheza fainali ya mashindano haya na timu ya Express kutoka nchini Uganda ambayo usiku wa jana ilitinga hatua ya fainali baada ya kuifunga KMKM ya visiwani Zanzibar mabao 2-1 kwenye dimba la Chamazi.