AUDIO: "Amepotea njia" - Mwakyembe

Saturday , 12th Aug , 2017

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amefunguka na kusema kuwa wajumbe 128 ambao leo wanachagua viongozi mbalimbali wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuchagua viongozi wenye kuendelea soka la Tanzania.

Mwakyembe amesema ili kuweza kupiga hatua mbele katika soka la Tanzania wajumbe wanapaswa kutumia vizuri nafasi zao kuchagua viongozi wenye maono, wazalendo na wasioteteleka kwa ushawishi wa muda mfupi. 

"Ndugu wajumbe viongozi bora huibuliwa na wajumbe makini wanaoongozwa na dhamira njema na uzalendo usioteteleka kwa vishawishi vya mpito, serikali inaamini tuna wajumbe makini huku ndani wasioyumbishwa na vishawishi vya muda na vishawishi vya mpito, tunataka viongozi wanaongozwa na uzalendo wa hali ya juu, hivyo tunataka viongozi bora wa TFF wenye hali, moyo, uelewa, weledi na uadilifu unaotakiwa kupeleka soka letu mbele" alisema Mwakyembe 

Aidha Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa yoyote ambaye anaona amegombea nafasi yoyote ndani ya TFF kwa lengo la kujipatia fedha au kutajirika basi anapaswa kutambua kuwa amepotea njia. 

Msikilize hapa Mwakyembe akifunguka zaidi.