Jumanne , 13th Jul , 2021

Afisa uhamasihaji wa  Yanga umeweka wazi kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba, wataipiga kwenye mshono ambao waliwashona walipokutana Uwanja wa Mkapa.

Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz.

Ikumbukwe kwamba Julai 3, Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga ulikuwa ni mchezo wa  ligi na mtupiaji alikuwa ni Zawad Mauya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo hii,afisa  Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wanakwenda kuwapiga wapinzani wao palepale kwenye mshono.

 “Tulikutana nao Uwanja wa Mkapa bila wachezaji wenye majina tukaamua mchezo kupitia Mauya, sasa tunakwenda kuwapiga palepale kwenye mshono''.

Simba na Yanga wanatarajiwa kukutana kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Lake Tanganyika ikiwa ni mchezo wa fainali, Julai 25.ya