Jumanne , 17th Mei , 2022

Mcheza Tenisi namba 6 Duniani Carlos Alcaraz amesema yupo tayari kushinda taji lake la kwanza kubwa la michuano ya Tenisi yani Grand Slam na hakuna cha kumkwamisha. Amesema haya kuelekea michuano ya wazi ya Ufaransa (French Open).

Carlos Alcaraz

Kinda huyo raia wa Hispania mwenye umri wa miaka 19 atakuwa akicheza kwa mara ya pili katika michuano ya wazi ya Ufaransa ambayo kwa mwaka huu yanaanza kutimua vumbi Mei 22, 2022. Mara ya kwanza alishiriki mwaka jana 2021 na aliishia raundi ya 3.

Kuelekea michuano ya mwaka huu amejinasibu kuwa yupo tayari kutwaa ubingwa wake wa kwanza wa Grand Slam, kwa sababu yupo vizuri kimwili na kiakili.

"Siogopi kusema niko tayari kushinda Grand Slam. Mwili najisikia vizuri sana. Nina nguvu kiakili. Mimi ni mchezaji hodari na mwishowe ndivyo inavyohitajika kushinda Grand Slam. Sasa nina kiwango bora, najisikia vizuri na kujiamini kabisa. Ni mambo mengi ambayo yanaweza kunivuruga na siogopi kusema niko tayari kushinda." amesema Carlos Alcaraz

Lakini atakuwa na kibarua cha kumvua ubingwa mchezaji namba moja Dunia Novak Djkovoc ambaye ndio bingwa mtetezi wa michuano hii na Djokovic anaiwania rekodi ya kutaka kushinda Grand Slam ya 21 ili amfikie Rafel Danal ambaye hapewi nafasi kubwa ya kushinda French Open mwaka huu.

Novak Djkovic bingwa mtetezi French Open 

Katika kalenda ya mwaka huu ya michezo ya Tenis Alcaraz ameshinda michuano ya Miami Open kwa kumfunga Casper Ruud lakini pia alimfunga Alexzender Zverev kwenye mchezo wa fainali wa michuano ya Madrid Open na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.