Abdul wa Serengeti awashangaza CAF

Friday , 19th May , 2017

Mchezaji wa Serengeti Boys, Abdul Suleiman aliyeibuka mchezaji bora katika mechi ya jana dhidi ya Angola amebainika hatumii dawa ya aina yoyote ya kusisimua misuli baada ya kufanyiwa vipimo.

Winga huyo aliwaweka kwenye wasi wasi maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kuonesha kiwango kikubwa cha uchezaji huku akiwa na pumzi za hali ya juu na kusababisha timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1.

Kitendo hicho kilisababisha kupelekwa katika vipimo mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa na kusababisha kushindwa kuenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora 'Man of the match' na matokeo yake ikabidi  awakilishwe na mlinzi Dickson Job