Wiki 118 za Barnaba na muonekano mmoja

Ijumaa , 21st Mei , 2021

Kama ilivyo kwa mavazi huja na mtindo fulani na kisha ku-trend kwa muda na baadae kupotea baada ya kuibuka aina nyingine ya mtindo, ndivyo ilivyo hata kwenye vitu vingine.

Msanii Barnaba

Moja ya mtindo wa nywele ulio-trend kipindi cha mwaka 2019 ni ‘dreadlocks’ karibu asilimia kubwa ya wasanii waliutumia lakini muda wake ulipoisha walizitoa rasta zao na kubaki na muonekano mpya.

Msanii Barnaba

Sasa inawezekana Barnaba Classic amenogewa nao kwani mpaka sasa ni wiki 118 zimepita kwa fundi huyu wa muziki akiwa na muonekano wa aina moja huku anachokifanya ni kubadilisha tu aina ya ufungaji wa rasta zake, muonekano huo aliutengeneza ikiwa ni maandalizi ya ku-sign dili la ubalozi na moja ya kampuni ya mawasiliano hapa nchini.