Jumatatu , 5th Aug , 2019

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili imekanusha juu ya taarifa inayosambaa mitandaoni ikimuonesha mwanamke mmoja mgonjwa anayedaiwa kujigeuza ndege usiku na kurudi kuwa binadamu asubuhi, aliyekamatwa na wagonjwa wenzake.

Mgonjwa anayedaiwa kujigeuza ndege

Taarifa hiyo ya Hospitali ya Muhimbili imesema kuwa imejiridhisha na uchunguzi uliofanyika na wamebaini kuwa picha na video hiyo hazihusiani na Hospitali ya Muhimbili kimazingira na katika takwimu zao hawana mgonjwa kama huyo.

"Kwanza hatuna mgonjwa huyo, pili, hatuna wodi zinazofanana na hiyo katika hospitali zetu (Upanga na Mloganzila), tatu, wauguzi wanaoonekana katika viso hiyo hawajavaa sare za hospitali yetu", imesema sehemu ya taarifa hiyo.

"Tunawaomba wananchi na watumiaji wa huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Upanga na Mloganzila) kutokuwa na hofu juu ya taarifa hizo kwani siyo za kweli", imeongeza taarifa hiyo.

Video inayosambaa mitanndaoni inamuonesha mwanamke huyo akiwa amezungukwa na wagonjwa, waangalizi wa wagonjwa na wauguzi kwenye wodi ya hospitali akikemewa na kutakiwa aondoke baada ya kukutwa na sintofahamu hiyo ya kujigeuza kutoka kuwa ndege hadi kuwa binadamu.

Isome hapa taarifa nzima.