Jumamosi , 7th Mei , 2022

Kutoka Lebo ya WCB msanii Zuchu amewajibu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kuwaambia wamewaonea kuifungia video ya mtasubiri aliyofanya na Diamond Platnumz.

Picha ya Diamond na Zuchu kwenye video ya Mtasubiri

Zuchu ameeleza hilo kwa kutuma ujumbe kupitia Instagram yake kwa kuandika 

"Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia. Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mmetuonea".

"Sisi ni vijana tunaotafuta riziki bila ya kuchoka lakini pengine wazazi wetu @basata.tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia, muda, vipaji na uwekezaji unaofanyika".

Zaidi msikilize hapa akizungumzia hilo.