Jumanne , 11th Mei , 2021

Youssou N'Dour,  huyu ni mwanamuziki kutoka nchini Senegal anatajwa kuwa ndiye msanii tajiri namba moja barani Afrika akiwa na utajiri wa dola milioni 145 – 150 hii ni kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na African Forbes 2021.

Pichani kutoka kushoto ni msanii Youssou N'Dour, Akon na 2 Baba (2 Face)

N'Dour alianza shughuli ya muziki miaka ya 70’s na ‘Mbalax’ ndio aina ya muziki anaoufanya na unapatikana kwao Senegal. 

Somo kubwa kutoka kwa Youssou N'Dour kwenda kwa wasanii wa Bongo Fleva ni kwamba, jamaa hana habari na mabadiliko ya kimuziki ambayo yamekuwa yakitokea kila uchwao, amebaki na aina ya kwao huko Senegal ambayo amedumu nayo kwa miaka na miaka.

Alishawahi kutajwa kwenye Tuzo za Grammy mara 6 na kushinda  mara 1, kitambo mno zaidi ya.miaka 20 nyuma na alishakuwa na Collabo za kimataifa na kina Wyclef Jean na Cannabis  miaka mingi iliyopita bila ya yeye kubadilika chochote.

Mwaka 2004, jarida la Rolling Stone lilimtaja Youssou N'Dour  kama mwimbaji mashuhuri aliye hai huko Senegal na sehemu kubwa ya Afrika.

Aliwahi kuwa Waziri wa Utalii Senegal kuanzia Aprili 2012 na alidumu mpaka Septemba 2013.

Orodha ya wasanii 10 matajiri Afrika

1.Youssou N'dour –  $145 Milioni
2.Akon – $80 Milioni
3.Black Coffee – $60 Milioni
4.Wizkid – $21 Milioni
5.Davido – $20 Milioni 
6.Don Jazzy – $18 Milioni
7.Burna Boy – $17 Milioni
8.2 Baba (2 Face) – $16.5 Milioni
9.Rude Boy – $16 Milioni
10.Timaya – $12 Milioni