Jumanne , 14th Apr , 2020

Katika hali isiyotarajiwa wasanii wa wawili kutoka lebo ya Kings Music Records ya msanii Alikiba, wametangaza kujitoa ndani ya lebo hiyo, na kuamua kufanya kazi zao binafsi.

Kushoto ni msanii Killy, kulia ni Cheed akiwa na Alikiba

Wasanii ambao wametangaza kujitoa ndani ya lebo hiyo ni Killy pamoja na Cheed, ambapo kupitia mtandao wa Instagram kila mmoja ameandika kuwa,

"Leo hii napenda kutamka kuwa mimi sio tena msanii wa Kings Music Records, nimeamua hili kwa akili yangu timamu kabisa, bila kushawishiwa na mtu yeyote na sijatumia kilevi chochote kile ni maamuzi yangu binafsi kwa ajili ya muendelezo wa mziki wangu, namshukuru sana Alikiba  kwa kila alichonifanyia na kujitolea kwa ajili ya mziki wangu, na sitoacha kumshkuru siku zote za maisha yangu naumia ila sina budi" ameandika Killy.

Aidha kwa upande wa Cheed yeye ameeleza kuwa  "Naitwa Rasheed maarufu kama Cheed, napenda kuwajulisha mashabiki zangu na watu wangu wote waliokuwa waki-support mziki wangu na wanaoendelea ku-upport kazi zangu kwamba, kuanzia leo hii mimi sio tena msanii wa Kings Music Records , nimeamua hili kwa akili yangu timamu kabisa bila kushawishiwa na mtu yeyote na sijatumia kilevi chochote kile, ni maamuzi yangu  binafsi kwa ajili ya muendelezo wa mziki wangu".