Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Msanii Kalapina ambaye alikuwa kwenye kundi la Kikosi cha Mizinga ambacho licha ya kazi za muziki wakizofanya, kilikuwa maarufu sana kwa ukorofi na ubabe.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Kalapina ametoa sababu ya wao kuwa na sifa hiyo mbaya ya ubabe na ukorofi kwa wasanii wengine na watu mbali mbali, na kusema walikuwa wanachukia miyeyusho iliyokuwa ikifanyika kwenye game.

"Sababu nyingi tu ikiwemo miyeyusho katika game, ambayo si tulikuwa tunaiona kitambo kile, lakini sasa hivi tunaweza kusema hiyo miyeyusho imekuwa mikubwa zaidi, kitu kama rushwa za kwenye industry, kimekuwa ni kitu cha kawaida sasa hivi, kiasi kwamba huangaliwi umekuja na ngoma kali, unaangaliwa umemwaga bei gani, watu wanakosa zile ladha za ngoma kali sasa hivi, kutokana na ambao wanatoa ngoma kali hawana uwezo wa kutoa hela, ndo uliuwa unasikia kikosi wagomvi, wakorofi, tulikuwa tunasimamia misingi na haki ambazo zinatakiwa zitetewe, mtu akizingua tunamzingua", alisema Kalapina.

Kalapina aliendelea kusema kuwa wao lengo lao kubwa lilikuwa ni kutetea game ichanue na ngoma kali ziende, na kupambana na ufisadi uliopo kwenye media.