Jumanne , 9th Mei , 2017

Mtayarishaji wa muziki wa bongo Fleva anayetamba na ngoma kibao kwenye masikio ya wapenda burudani, Mr. Ttouch amefunguka na kudai hawezi kukata tamaa katika kumsaidia rapa Young D na kwamba yeye hatazami tabia bali muziki mzuri.

Akifunguka kwenye story tatu ya Planet Bongo East Africa radio, Touch amesema kwamba amejitoa kufanya kazi na Youung Dee na kwa kuwa wao ni vijana hakuna kitakachomshinda hivyo hawezi kuacha kipaji kipotee kwa sababu ya tabia tu anazozisikia kutoka kwa watu.

"Mziki unampa dhamana mtu haijalishi ulikuwa wapi na unatoka wapi. Siyo sawa kuacha kitu kizuri kikawa kinaelea mtaani pasipo kukipatia msaada, kazi yetu ni kutengeneza kazi nzuri ili watu wakiwa kwenye magari yao hata wakienda club wacheze muziki wetu. Hayo mambo mengine mimi siangalii nachoangalia ni muziki wangu kwa sababu ni kazi yangu mimi"- Mr. Ttouch alifunguka.

Young Dee ambaye yupo chini ya uongozi wa 'King Cash' iliyo na mkono wa Mr TTouch anahofiwa na mashabiki pamoja na watu mbalimbali kurudi kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kitu ambacho Mr. Ttouch amekuwa akikipinga mara kwa mara.

Msikilize akifunguka hapa chini zaidi,