Jumatano , 12th Mei , 2021

The Black Butterfly msanii Mwasiti ametoa 'comment' yake baada ya kutoka kwa takwimu mpya za Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kusema takwimu hizo zinatisha na ilipofikia sio sehemu nzuri.

Picha ya msanii Mwasiti

"Takwimu kama hizi zinatisha sana sio kidogo, sasa hii ni ya Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ukiletewa ya ujauzito ndio eehh 'Mungu baba', vijana tuwe makini dunia imebadilika, tutulie na tufanye maamuzi sahihi kwa wakati sahihi"

"Asilimia kubwa ya vijana mambo yao yanafanana, tuambiane ukweli kwa sababu tulipofika sio sehemu nzuri ya kujivunia, vinginevyo kama hatuongei athari itakuwa kubwa zaidi ya tunavyofikiria, miaka 14 mpaka 24 ni vijana wadogo wanaoambilika, hili janga lipo tusichukile poa".

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dkt Dkt. Leonard Maboko ambapo amesema kuna changamoto mpya ya maambukizi hayo kwa vijana wa miaka 15 mpaka 24.