Picha ya msanii Spack Tz
Spack amesema kuna maneno mengi yamezungumzwa kuhusiana na yeye kipindi ambacho amekaa kimya kwa muda mrefu ila binafsi hajawahi kukaa na jambo rohoni mwake.
"Kuna maneno na mambo mengi yamekuwa yakiendelea lakini binafsi sijawahi kuweka kitu katika roho na kama kuna vitu vingine nyuma sikuvijua, maneno hayo nimeyasikia ila sijamuona wa kumuhukumu"
"Binaadam wa kawaida hana nguvu ya kustopisha yanayoendelea kwamba nisisemwe, kama kuna mtu anasema nimerogwa ni yeye atajua mwenyewe yote kwa yote najijua kama nipo" ameeleza msanii Spack
Interview nzima bonyeza hapo chini kutazama.