Sio dhambi - Goodluck Gozbert

Saturday , 12th Aug , 2017

Staa wa muziki wa Injili, Goodluck Gozbert, amefungka na kusema hajutii kuwatungia nyimbo za mapenzi baadhi ya wasanii maarufu hapa nchini na kusema kufanya hivyo si dhambi.

Goodluck Gozbert

Gozbert amesema katika maisha suala la mapenzi limetawala, hivyo kitendo chake cha kutunga hakiendi kinyume na imani yake.

“Unajua suala la mapenzi lipo ndani ya jamii yetu, kutunga nyimbo zinazozungumzia jambo hilo siendi kinyume na Imani yangu,” alisema.

Gozbert ndiyo msanii aliyemwandikia wimbo Ommy Dimpoz wimbo wake mpya 'Cheche' lakini pia ameshawahi kumuandika msanii Ben Pol wimbo 'Moyo Mashine' pia ameandika nyimbo kadhaa za msanii Mo Music, mbali na kuimba nyimbo za injili na utunzi wa nyimbo mbalimbali lakini pia ni mtayarishaji wa muziki . 

Itazame hapa video ya wimbo wake mpya  unaoitwa 'Shukurani "