Rammy Galis
Rammy amesema kwamba yeye ataendelea kufanya kazi kubwa ili kuhakikisha kipaji chake kinakuwa na ndio maana hata maandalizi ya filamu yake ya 'Hukumu', ametumia muda mrefu kuiandaa ili kupata kitu kizuri na kuweza kuwapatia mashabiki zake kitu ambacho kitawaridhisha.
Katika uzinduzi wa filamu yake Rammy Galis aliongozana na mtoto wa marehemu Agnes Masogange aliyetambulika kwa jina la Samiya na kusema kwamba "muvi yangu hii niliigiza na marehemu Masogange na kwa kuwa marehemu aliacha familia mtoto wake na baba yake basi mauzo yatakayopatikana nitapeleka nusu kwa mtoto pamoja na baba wa marehemu Masogange".
Baba Samiya ambaye ni mzazi mwenza wa Masogange amesema anamshukuru Rammy kwa kuruhusu asilimia ya mapato ya filamu yake iende kwa familia ya Masogange, Mtoto na Babu na kusema suala la mtoto wake kuanza kuigiza atamruhusu baada ya kumaliza masomo ya sekondari ambapo anaamini atakuwa tayari ameshajitambua.